KUTAFAKARI NI SHUKURANI “ Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” Flp 4:8 SUV Ninapoweka mda wa kutafakari, kufikiri mambo yote mema, vitu vyote vyema, maneno yote mema ambayo Mungu, Bwana, Mfalme, Roho Mtakatifu, na Baba yetu ametufanyia na kututendea ni Kutembea katika Moyo wa Shukurani, kwani huwezi kutafakari pasi na kuzingatia. Na hii ni pamoja na mambo yote mema, vitu vyote vyema ambavyo Wana wa Mungu na watu wanavyotutendea na kutufanyia. Kutafakari Ni Shukurani Kuzingatia Ni Kuonesha Umuhimu Na Uthamani “ Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; s...